Vijana Tanzania Hawajaathirwa na Changamoto ya Afya ya Akili – Ripotii

,

Ripoti mpya ya kimataifa imeitaja Tanzania kushika nafasi ya tano duniani kwa kuwa kizazi cha vijana ambao hawajaathiriwa na changamoto ya afya ya akili, ikizipita nchi za Ulaya, Amerika, Asia na Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa Washington DC kufuatia utafiti uliofanywa na taasisi ya Sapien Labs, vijana barani Afrika wameonyesha kuwa na uimara wa afya ya akili wakati dunia ikishuhudia ongezekoo kubwa la changamoto ya afya ya akili miongoni mwa vijana duniani.

Tanzania imetajwa kushika nafasi ya tano duniani huku Ghana ikishika nafasi ya kwanza kidunia, na kufuatiwa na Nigeria, Kenya, Zimbabwe, hivyo kufanya nchi zote tano za kwanza kutoka barani Afrika.

Ripoti ya Dunia ya Afya ya Akili 2025 (The Global Mind Health Report 2025) inaonesha nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kuzipita nchi nyingi zenye kipato cha juu, huku ikionesha kuongezeka kwa tatizo la afya ya akili miongoni vijana duniani.

Utafiti huo uliotumia data zilizokusanywa kutoka watu zaidi ya milioni moja katika nchi 84 umeonyesha asilimiia 41 ya vijana walio katika umri wa utu uzima ambapo wamezama katika matumizi ya teknolojia za kidigitali, wakitegemea intaneti kwa mawasiliano, elimu, burudani na maingiliano ya kijamii (umri kati ya miaka 18-34) duniani wanakabiliwa na changamoto ya afya ya akili.

Ripoti hiyo inaonesha kuporomoka kwa uwezo wao wa ufahamu, kijamii, kushindwa kudhibiti mihemko na kupungua kwa uwezo wa kimwili ambavyo kwa kiasi kikubwa vimethiri uwezo wao wa kupambana na changamoto za maisha.

Kwa upande mwingine, ripoti hiyo inaonesha tofauti ya kikanda kwa tatizoz la afya ya akili(regional) huku baadhi ya nchi za Afrika zikiongoza kwa kupata alama za juu katika matokeo ya afya ya akili kwa vijana.

Kwa mfano, vijana waliofikia umri wa utu uzima katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara wameonesha kuwapita wenzao wanaoishi kwenye nchi zenye kipato cha juu zikiwemo za Amerika ya Kusini, Ulaya na sehemu za Asia.

Hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2,000 kundi la umri wa vijana iliohusisha utafiti huo (miaka 18-34) lilifanya vizuri katika ustawi na hali nzuri ya afya ya akili likilinganishwa na makundi mengine ya umri.

“Leo hii hali imegeuka, vijana watu wazima wako katika hatari mara nne zaidi ya wale wenye umri wa zaidi ya miaka 55 kupata changamoto ya afya ya akili yenye kuhitaji matibabu, hali ambayo kwa kiasi kikubwa imeathiri uwezo wao kuzalisha katika maisha yao ya kila siku.” Inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Ripoti ya Afya ya Akili Duniani 2025 imehusisha badiliko hilo na sababu kadhaa zikiwemo matumizi ya mapema ya simu za kiganjani wakati wa utoto, kuongezeka kwa matumizi ya vyakula na vinywaji vinavyotengenezwa viwandani kama vile soda, vyakula vilivyogansishwa na vinavyohifadhiwa kwenye vifunashio, kuporomoka kwa uhusiano wa karibu katika familia na kutothamini mambo ya kiroho.

Sapien Labs ni taasisi isiyo ya faida iliyojikita katika kuelewa athari mabadiliko ya kasi ya kijamii, kiteknolojia, na mazingira ya kemikali katika ubongo na akilil ya mwanadamu. Mradi wao wa Global Mind Project ndio mkubwa zaidi unaofuatilia vipengele 47 ya afya ya akili na sababu nyingine za kimaisha na kimazingira katika nchi zaidi ya 85 kwa lugha 25.

Taasisi hiyo inaongozwa na wataalamu wa sayansi ya neva na mishipa ya fahamu, saikolojia na wale wa sayansi ya kompyuta katika kuchambua na kutatua masuala magumu ya kisayansi walikusanya data kupitia utafiti wa kimtandao uliofanywa Asia, Africa, Ulaya na Amerika.

“Hatari ya tatizo ya afya ya akili inaonekana kuwa endelevu kutoka kizazi hadi kizazi na linakwenda mbali zaidi ya kuongeza viwango vya juu vya mfadhaiko na wasiwasi,” alisema Prof Tara Thiagarajan, kiongozi wa waandaaji wa ripoti hiyo na mwanzilishi na mwanasayansi mkuu wa Sapien Labs.

“Tumetathimini uwezo wa aina mbali mbali ambao mtu anapaswa kuwa nao ili kukabili chanamoto za maisha na kugundua kuwa vijana wengi walio katika umri wa utu uzima wanahangaika.

Pamoja na mifadhaiko na wasiwasi, mara nyingi wanakumbana na changagmoto za kudhibiti mihemko, kushughulikainjdwa kumudu uhusiano na wengine, na kupoteza uwezo wao wa kuelekeza akili zao katika jambo bila kuvuruga mawazo,”

Kwa mujibu wa utafiti huo, kufanya vizuri kwa baadhi ya nchi za Afrika kunaweza kumaanisha kuwa mambo ya kijamii na kifamilia yanayokuza uimara na ustawi na kupunguza athari mbaya kama vile msongo wa mawazo au sababu hatarishi vinaweza kuwa vinachangia vizuri kwenye matokeo hayo.

Matokeo ya utafiti huo yanaonesha pia kuwa vijana walio katika umri wa utu uzima Kusini mwa Jangwa la Sahara wameripotiwa kuwa na uimara wa kiroho, kuchelewa kuanza matumizi ya simu za kiganjani wakati wa utoto na kuwa na uhusiano wa karibu wa kifamilia ukilinganisha na wenzao katika nchi tajiri.

Tanzania, kwa mfano, imeshika nafasi ya juu kabisa kidunia katika kipimo cha mambo ya kiroho na ndio yenye wastani wa juu wa umri wa watu waliochelewa kuanza matumizi ya simu za kiganjani licha ya kushuka kutoka nafasi ya kwanza mwaka jana hadi ya tano mwaka huu.

Kenya na Nigeria pia miongoni mwa nchi ilizoshika nafasi ya juu kidunia, huku Kenya ikionesha kufanya vizuri zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Licha ya tofauti za kikanda, tofauti ya afya ya akili kati ya wazee na vijana imeendelea duniani kote, huku wazee wakionesha kuwa na afya imara zaidi ya akili kuliko idadi ya vijana.

Utafiti uliotangulia wa Sapien Labs ulionesha kuwa tofauti hiyo ilianza kukua kabla ya mwaka 2020 na kuongezeka kwa kiasi kikubwa wakati wa janga la UVIKO-19 2020 na 2021, wakati ambao afya ya akili ya vijana wenye umri wa utu uzima (miaka kati ya 18 na 34) ilishuka kwa kasi, huku vizazi vya umri mkubwa vikiathirika kwa kiasi kidogo tu.

“Kwa miaka mitano iliyopita, tofauti hii kwa kiasi kikubwa haijabadilika,” alisema

Dr Thiagarajan, na kuongeza kuwa waandaaji wa sera wanapaswa kutazama kwa karibu athari pana za kiuchumi za kuongezeka kwa vijana wanaoingia katiika kundi la nguvukazi wakiwa na afya dhaifu ya akili,” alisema.

Huku ikigusia sababu nyinginje nyingi za kushuka kwa afya ya akili, ripoti hiyo inabainisha sababu nne za msingi zinazochangia changamoto ya afya ya akili kwa vijana duniani. Imezitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na matumizi ya mapema ya simu wakati wa utoto, ongezeko la vyakula vya viwandani, kupunggua uhusiano wa kifamilia na kutojali mambo ya kiroho. Kila moja ya sababu hizi inahusishwa na ongezeko la hatari matatizo ya afya ya akili na kupungua kwa uwezo wa vijana kuyakabili mahitaji ya maisha.“

Nchini Marekani, matumizi ya fedha kwa ajili ya utafiti wa afya ya akili na uangalizi yameongezeka sana kwa mabilioni ya dola, kama ilivyo kwa nchi za mashariki.

Na wakati hilo ni muhimu, halileti mabadiliko ya kuonekana,” alisema. “tuhahitaji kuacha kupambana na dalili na badala yake kupambana na matatizo makubwa zaidi yanayoathiri uzalishaji na ustawi wa vijana duniani.

Kwa mfano, hatua za kisera zinazodhibiti upatikanaji wa simu za kiganjani kwa watoto na matumizi ya vyakula vya viwandani vinasaidia kulinda afya ya akili ya kizazi cha vijana bila hivyo, uchumi wa dunia utatapatapa kwa miongo kadhaa ijayo.”

Ripoti hiyo pia imabainisha hatua mahususi za kisera zinazoweza kupunguza madhara, hasa madhara yanayosababishwa na matumizi ya mapema ya simu za kianjani kuongezeka kwa matumiizi ya vyakula vitokavyo viwandani.

Kwa masuala yanayohusishwa na simu za kiganjani, ripoti hiyo imeshauri utungwaji wa sera zinazozuia matumizi yake wakati wa muda wa masomo na kuanzishwa kwa sharti la kuweka umri maalumu wa kutumia mitandao ya kijamii.

Kuhusu vyakuka vinanvyoandaliwa viwandani, ripoti hiyo imetaka kuwepo kwa uwekezaji mpya katika tafiti ambazo zinaweza kufichua hatari zinahusishwa na aina mbalimbali za rangi, vikolezo, dawa za kuzuia vyakula visioze na vitu vinavyotumika kugandisha vyakula pamoja na viungio vingine vinavyopatikana kwenye vyakula na kuleta ushahidi utakaounga mkono uanzishwaji wa kanuni za kupunguza matumizi yake.

“Wakati ripoti hii si ya kwanza kuhusisha vitu hivi na changamoto za afya ya akili, upana na kina cha data ilizofanyiwa kazi na Global Minds zitasimama kuonesha ukubwaa wa matatizo vinayosababisha,” alisema Prof David Blachflower, profesa wa uchumi katika Chuo cha Dartouth.

“Kwa sababu pale unapoona ushahidi kuwa karibu nusu ya vijana wote duniani moyo wa nguvu kazi wanapambana na mlolongo wa chanamoto za afya ya akili, hii ina maana tunakabiliwa na hatari inayoweza kudhoofisha afya ya uchumi wote na jamii.

Ni kiashiria cha wazi kuwa tunahitaji kuchukua hatua kushughulikia mzizi wa tatizo.”