:::::::::::
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), imetangaza kusitisha kwa muda safari zake za kwenda na kutoka Dubai, kutokana na kufungwa kwa anga la Mashariki ya Kati.
Katika taarifa kwa wateja iliyotolewa leo Februari 28, 2026, kampuni hiyo imesema imesitisha safari hizo hadi itakapotolewa taarifa nyingine na kwamba inaendelea kufuatilia kwa karibu hali ilivyo na mara tu hali itakapothibitishwa kuwa salama na thabiti basi safari hizo zitarejea mara moja.
Aidha, ATCL imewaomba radhi abiria waliokata tiketi za safari, ikiwaahidi kuwapa fursa ya kukata tiketi tena bila malipo ya ziada ikisisitiza kuwa usalama wa abiria, wafanyakazi na ndege kwa ujumla ndiyo kipaumbele chao.
