Global Publishers
February 28, 2026
0 Comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Emmanuel Nchimbi, na Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, leo Februari 28, 2026 wameungana na waombolezaji kushiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Marehemu Polycarp Pengo.
Misa hiyo inafanyika katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria – Pugu, jijini Dar es Salaam, huku mamia ya waumini na viongozi mbalimbali wakihudhuria kutoa heshima zao za mwisho.

