IRGC Yadai Kulipiza Kisasi Baada ya Kifo cha Khamenei, Trump Atoa Onyo Kali

Global Publishers
March 1, 2026
0 Comments

Taarifa zinazodaiwa kuenea mitandaoni, mashirika ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ikiwemo Jeshi la Mapinduzi la Kiislamu (IRGC), wametangaza kuwa watafanya mashambulizi makali dhidi ya Marekani.

Habari hizo zinadai kuwa hatua hiyo itatokana na kile kinachodaiwa kuwa kifo cha Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa Rais wa Marekani, Donald J. Trump, ametuma onyo kali kwa Iran kupitia mtandao wake wa Truth Social, akisema kuwa Marekani itachukua hatua kali kisiasa na kijeshi ikiwa Iran itatekeleza mashambulizi dhidi yake.

Katika ujumbe huo unasemekana Trump amelionya Jeshi la Mapinduzi la Iran na serikali ya Tehran kuwa wataadhibiwa kwa nguvu isiyowahi kutumika hapo awali iwapo watatekeleza vitisho vya mashambulizi.