MBUNGE KOOLA ASHIRIKI MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR’AN – HIMO

VUNJO. 

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Enock Koola amewapongeza walimu wa madrasa kwa juhudi zao za malezi ya kiroho na maadili kwa watoto na vijana kupitia elimu ya dini. 

Koola ametoa kauli hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kuhifadhi Qur’an yaliyofanyika mji wa mdogo wa Himo ambapo aliwapongeza washiriki wote kwa nidhamu, juhudi na kujituma katika mashindano hayo muhimu kwa ustawi wa jamii.

Mbunge aliwahimiza vijana kuendelea kushikamana na misingi ya imani, kuzingatia masomo yao darasani pamoja na kuepuka makundi yenye mienendo hatarishi ili kujenga jamii salama na Taifa lenye kizazi chenye maadili mema.

Katika kuhitimisha hafla hiyo, Koola alikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano, vyeti kwa washiriki wote, pamoja na zawadi maalum kwa walimu na majaji waliowezesha kufanikisha mashindano hayo.