Vigogo wa Iran waliouawa na Marekani-Israel

Kufuatia kuthibitishwa kwa mauaji ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, vyombo vya habari vya serikali nchini humo vimethibitisha kuuawa kwa viongozi kadhaa waandamizi wa serikali na familia ya Khamenei.

Miongoni mwa waliouawa katika shambulizi la Jumamosi ni pamoja na Ali Shamkhani, mshauri wa usalama wa Khamenei, Jenerali Abdolrahim Mousavi, Mkuu wa Majeshi ya Iran, Aziz Nasirzadeh, Waziri wa Ulinzi na Mohammad Pakpour, Kamanda Mkuu wa IRGC.

Shirika la habari la IRNA limesema makamanda wengine wa jeshi pia wameuawa na majina yao yatatangazwa baadaye.
Mbali na viongozi hao waandamizi wa Iran kuuawa, binti wa Khamenei pamoja na mjukuu wake pia, waliuawa katika mashambulizi hayo.