WAZIRI MKUU AWAAGIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUANDAA JEDWALI LA UTEKELEZAJI UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza watendaji wa Serikali kuandaa jedwali la kuonesha namna walivyotatua kero za wananchi katika kila wiki ya mwisho wa mwezi.

Amesema hayo leo Jumapili (Machi 01, 2026) katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi za Zamani, Babati Mjini mkoani Manyara.

Amesema kuwa Serikali haiwezi kukubali utaratibu wa kulimbikiza matatizo ya watu kana kwamba Serikali haipo.

Ameongeza kuwa Serikali imetengeneza utaratibu ndani ya nchi wa kuwa na uongozi katika kila eneo kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi kupata ufumbuzi wa matatizo yao.

“Hatukutengeneza ofisi hizi za Serikali ili kugawana vyeo. Ninawahakikishia tukianza kufuatilia tutajua nani anaweza kazi na anastahili kukaa ofisini.”