Mhe Senyamule ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Machi 2,2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu jambo waliloandaa la utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi wa Dodoma kama ambavyo yamekuwa ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, maelekezo ya vitendo ya Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba na maelekezo mahsusi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Prof.Riziki Shemdoe ambayo yamekuwa yakisisitiza utatuzi wa kero za Wananchi.
“Taasiisi zote za Umma zilizopo katika Mkoa wa Dodoma zitakuwepo pale Nyerere Square kwa siku tatu kusikiliza nakutatua kero za wananchi,kwahiyo ni wito wangu kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma kujitoleza kuja kutumia fursa hii adhimu ambayo tumeiweka ili kuwarahishia kwani Taasisi zitakuwepo pale kutoka upande wa afya,maji na hata miundombinu”.
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo ameainisha huduma tatu muhimu zitakazotolewa katika viwanja hivyo kwa siku hizo 3, kuwa ni kusikiliza kero za wananchi ambapo Taasisi zote za Umma zitashiriki kazi hii Pia kutoa Taarifa kwa Umma wa Wana Dodoma na Taifa kwa ujumla juu ya kazi iliyofanywa katika siku 100 za Dkt Samia akiwa madarakani katika awamu ya sita na muhula wake pili.
Ambapo tatu ni utoaji wa huduma bure kwa wananchi kama vile upimaji wa magonjwa ikiwemo sukari na presha pamoja na kuwepo kwa huduma za ki hiari za kutoa damu kwa watakaopenda ambapo huduma hizi zimeunganiswa ili kuwa fursa kwa wananchi wakati wa utatuzi wa kero zao.
Pamoja na hayo pia ametoa wito kwa Taasisi za Umma na Watumishi wake katika Mkoa wa Dodoma kuhakikisha kwamba kila mmoja anawajibika kusikiliza kero za wananchi kwani kama Mkoa wanategemea kutengeneza mfumo kuanzia ngazi za chini za Vitongoji mpaka ngazi ya Mkoa, mfumo wa kupata Taarifa za kero zinazosikilizwa na utatuzi wake katika ngazi zote na kuzitolea Taarifa kila mwezi.