Bakari Mahundu
March 4, 2026
0 Comments
Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Dkt. Salum Soud Hamed, amefanya ziara maalum wilayani Kisarawe akiongozana na Kamati ya Utalii na Biashara, kutembelea shamba la kisasa la uzalishaji wa kuku wa mayai linalomilikiwa na kampuni ya @afi_green
Ziara hiyo imelenga kujifunza na kujionea fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na ufugaji, hususani ufugaji wa kuku wa mayai, kama njia ya kuongeza ajira na kukuza uchumi. Dkt. Hamed ameonesha nia ya kuwakaribisha wawekezaji hao Zanzibar ili kuwekeza na kutoa elimu kwa wananchi, hatua itakayochochea ajira kwa vijana.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Fatma Mandoba, amewapongeza Afi Green kwa kuwaajiri wazawa wa Kisarawe na kuwataka vijana wa Zanzibar kutotegemea sekta ya utalii pekee, bali kuchangamkia fursa za ufugaji wa kuku wa mayai zenye tija kubwa kiuchumi.
Katika shamba hilo, zaidi ya kuku wazazi 50,000 wanatunzwa, wakizalisha vifaranga kati ya 500,000 na 600,000 kila mwezi, sawa na wastani wa vifaranga milioni sita kwa mwaka.