Video: Marekani Yatangaza Mpango wa Kuchukua Udhibiti wa Anga ya Iran

Global Publishers
March 4, 2026
0 Comments

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, amesema Marekani na Israel zinakusudia kuchukua udhibiti kamili wa anga ya Iran ndani ya muda mfupi, kama sehemu ya operesheni zao za kijeshi zinazoendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 4, 2026 Hegseth alisema kuwa ndani ya wiki moja, mataifa hayo mawili yatakuwa na udhibiti wa anga ya Iran.

“Natumaini wote wanaotazama wanaelewa maana ya anga udhibiti kamili wa anga,” alisema.
“Inamaanisha tutaruka mchana na usiku, tukitafuta, kubaini na kuharibu makombora na miundombinu ya viwanda vya kijeshi vya Iran.”

Aliongeza kuwa, kwa mtazamo wa Washington, Iran “haitaweza kufanya chochote kuzuia hilo.”