ALHIKMA FOUNDATION YATANGAZA MASHARTI 10 YA NDOA 130

::::::::

Msharti 10 yaliyotangazwa na Taasisi ya Al-Hikma ili kutimiza kigezo cha kufanikisha mchakato huo. 

Miongoni mwa masharti hayo yaliyotangazwa na mkurugenzi wa taasisi hiyo, Sheikh Nurdin Kishki ni pamoja na mwanamke ndio akachukue fomu ya mchakato huo, awe Mtanzania, muombaji asiwe na mume na huyo mtarajiwa wake asiwe na mke. 

Mengine ni awe ameposwa na kukubaliwa, mwanaume awe na chanzo cha kupata riziki, awe amejaza fomu na kupita kwenye usaili, awe tayari kufunga ndoa ya pamoja, athibitishwe na imamu wa eneo lake kwa barua na kitambulisho cha Taifa na mzazi wa mwanamke akubali ndoa hiyo itafungwa pamoja na wengine. 

Sheikh Kishki ametoa utaratibu huo leo Alhamisi Machi 5, 2026 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuhusu mashindano ya Quran yaliyofanyika Machi Mosi, sambamba na kutoa shukurani kwa watu waliojitolea kufanikisha mchakato huo. 

Utaratibu wa kulipia mahari ulitangazwa na Sheikh Kishki siku ya kilele cha mashindano ya mabara ya kuhifadhi Quran tukufu yaliyofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo vijana 130 watalipiwa mahari.