Halmashauri ya Jiji la Mbeya Yatangaza Nafasi 19 za Ajira

Global Publishers
March 5, 2026
0 Comments

Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na tisa (19) baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kumb. Na: MCC/E.40/5/VOL. II/85
Tarehe: 04/03/2026

1.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 13

Ngazi ya Mshahara: TGS B

Majukumu

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari

  • Kusafirisha watumishi kwenye safari za kikazi

  • Kufanya matengenezo madogo madogo

  • Kusambaza nyaraka mbalimbali

  • Kujaza na kutunza daftari la safari

  • Kufanya usafi wa gari

  • Kazi nyingine atakazopangiwa na Mwajiri

Sifa za Mwombaji

2.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 6

Ngazi ya Mshahara: TGS C

Majukumu

  • Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka

  • Kusambaza na kupokea majalada

  • Kutafuta na kurejesha kumbukumbu

  • Kufuatilia mzunguko wa majalada (file tracking)

  • Kazi nyingine atakazopangiwa

Sifa za Mwombaji

Masharti ya Jumla

  • Awe raia wa Tanzania (miaka 18–45)

  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba

  • CV yenye anuani, simu, barua pepe na wadhamini watatu

  • Viambatisho vyote viwe vimethibitishwa na Mwanasheria/Wakili

  • “Result slip” na Testimonial hazitakubaliwa

  • Waombaji waliosoma nje ya nchi wathibitishe vyeti (TCU/NACTE/NECTA)

  • Maombi ya kughushi yatachukuliwa hatua za kisheria

  • Maombi yaandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza

Mwisho wa kutuma maombi: 17/03/2026

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal):
👉 https://portal.ajira.go.tz/

Barua ziandikwe na kuelekezwa kwa:
Mkurugenzi wa Jiji
Halmashauri ya Jiji la Mbeya
S.L.P 149
Mbeya

📍 Ofisi Kuu: Mtaa wa Maktaba, Mbeya
📞 Simu: +255 25 2502372
📠 Nukushi: +255 25 2502488
📧 Barua pepe: [email protected]
🌐 Tovuti: www.mbeyacc.go.tz