Dar es Salaam Kuna ushindi wa kupiga picha na kuonyesha watu. Halafu kuna ushindi wa aina nyingine. Ule unaokupa mwendo mpya kwenye maisha.
Daniel Deogratus Sambo, mjasiriamali wa Kigoma Mjini, amesema amepata mwendo huo baada ya kushinda pikipiki aina ya TVS kupitia kampeni ya #ShindaBoda ya PigaBet. Kwa Sambo, boda hii si zawadi ya kuitazama tu. Ni mchongo wa kufanya kazi zisogee na kipato kiongezeke.
“Nilianza kucheza muda mrefu, lakini leo nimebahatika kushinda pikipiki. Hii itanisaidia sana katika biashara zangu za kila siku,” alisema Sambo.
Kwa lugha ya Bongo, Sambo anasema hii ni kama kupewa mchongo wa kusukuma mambo. Inarahisisha shughuli, inaokoa muda, na inapunguza stress za usafiri. Hapo ndipo kauli ya #ShindaBoda inapokaa vizuri. Kuwa boss si lazima uwe na ofisi. Kuwa boss ni pale unapopata namna ya kujisimamia na kuongeza kipato.
Katika tukio hilo, mshindi mwingine Doreen Massawe naye alisema ushindi wake unaenda kubeba uzito wa kazi. Doreen, anayejihusisha na kilimo, amesema boda hiyo itamsaidia kurahisisha shughuli zake na kuongeza ufanisi wa kila siku.
“Ninajihusisha na kilimo, hivyo pikipiki hii itanisaidia sana kwenye shughuli zangu,” alisema.
Akizungumzia kampeni hiyo, Afisa Masoko wa PigaBet Tanzania, Hemed Msonge, alisema #ShindaBoda inatoa pikipiki mbili kila wiki kwa muda wa wiki sita. Alisisitiza kuwa ushiriki unapaswa kuwa wa uwajibikaji.
“Tunahimiza Watanzania kuendelea kushiriki kwa uwajibikaji. Droo zinaendelea kila wiki hadi mwisho wa kampeni,” alisema.
Kwa Sambo, ujumbe ni mmoja. Kuna zawadi, na kuna mchongo. Na hii ni mchongo wa kusukuma maisha.
18+ | Cheza kwa uwajibikaji.
