Waziri Kombo Atembelea Ubalozi wa Iran Kutoa Salamu za Pole Kifo Cha Khamenei – Video

Bakari Mahundu
March 5, 2026
0 Comments

Waziri Kombo Akisaini Kitabu Cha Maombolezo Ubalozi Wa Iran Tanzania, Kufuatia Kifo Cha Ali Khamenei

DAR ES SALAAM, Machi 4, 2026 — Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania umempokea Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyefika katika Makazi ya Balozi wa Iran jijini Dar es Salaam kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha Ali Khamenei.

Waziri Kombo aliwasilisha salamu hizo kwa niaba ya Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akionesha mshikamano wa Serikali na wananchi wa Tanzania katika kipindi hiki cha maombolezo.
Ubalozi wa Iran umeishukuru Serikali ya Tanzania kwa ujumbe huo wa faraja na mshikamano mkubwa.

Aidha, Kitabu cha Maombolezo kimefunguliwa katika Makazi ya Balozi wa Iran nchini, na viongozi, wanadiplomasia pamoja na wadau mbalimbali wanaendelea kufika kuandika salamu zao za rambirambi.