CHAMA cha Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi Tanzania (TUCASA) kimeiomba Serikali kuanzisha sheria maalum ya malipo katika sekta ya ujenzi ili kusaidia kuimarisha mazingira ya kazi kwa makandarasi wa ndani na kuhakikisha wanapata malipo kwa wakati wanapotekeleza miradi ya maendeleo ya umma.
Chama hicho kimesema kuwa uwepo wa sheria hiyo utasaidia kuweka utaratibu wa wazi wa malipo na kupunguza changamoto ya ucheleweshaji wa fedha, hali ambayo kwa sasa inaathiri uwezo wa kifedha wa makandarasi wengi wa ndani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 06, 2026 Mwenyekiti wa TUCASA, Qs Samuel Marwa amesema sheria hiyo inayojulikana kimataifa kama Security of Payment Act inaweza kusaidia kuweka mfumo wa kisheria unaolazimisha malipo ya kazi za ujenzi kufanyika ndani ya muda maalum pamoja na kuweka utaratibu wa haraka wa kutatua migogoro ya malipo.
Ameeleza kuwa ucheleweshaji wa malipo ya kazi zilizokamilika na kuthibitishwa umekuwa changamoto kubwa inayokwamisha ukuaji wa makandarasi wa ndani na kupunguza uwezo wao wa kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.
Marwa amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo, wakandarasi wengi hulazimika kukopa fedha katika taasisi za kifedha kwa riba kubwa ili kuendelea na utekelezaji wa miradi waliyopewa na taasisi za umma.
Kwa mujibu wa Marwa, hali hiyo huongeza gharama za miradi na wakati mwingine husababisha baadhi ya kampuni kushindwa kuendelea na shughuli zao au hata kufilisika kutokana na mzigo wa madeni unaotokana na kuchelewa kwa malipo.
Aidha, TUCASA imeeleza kuwa uzoefu wa kimataifa unaonyesha kuwa uwepo wa sheria kama hiyo husaidia kuimarisha mtiririko wa fedha katika sekta ya ujenzi na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi.
Amebainisha kuwa sheria kama hiyo tayari inatumika katika nchi mbalimbali zikiwemo Australia, Uingereza, Singapore na Malaysia ambapo imechangia kuimarisha sekta ya ujenzi na kulinda maslahi ya wakandarasi.
Chama hicho pia kimeipongeza Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa kuimarisha ushiriki wa makandarasi wa ndani katika miradi mikubwa ya maendeleo ya miundombinu nchini.
Pia kimetambua kauli ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba aliyoitoa Februari 15, 2026 mkoani Tanga alipokuwa akizungumza na wadau wa mradi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP), ambapo alisisitiza umuhimu wa kulinda fursa za makandarasi wa ndani.
Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alionya dhidi ya baadhi ya makampuni ya kigeni yanayotumia majina ya Watanzania kusajili kampuni ili kupata zabuni za Serikali kinyume na taratibu.
Hata hivyo, TUCASA imesisitiza kuwa kuanzishwa kwa sheria ya malipo pamoja na maboresho ya mifumo ya manunuzi ya umma kutasaidia kujenga sekta imara ya ujenzi, kuongeza ushindani wa haki na kuhakikisha makandarasi wa ndani wanashiriki kikamilifu katika maendeleo ya miundombinu na uchumi wa taifa.CHAMA cha Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi Tanzania (TUCASA) kimeiomba Serikali kuanzisha sheria maalum ya malipo katika sekta ya ujenzi ili kusaidia kuimarisha mazingira ya kazi kwa makandarasi wa ndani na kuhakikisha wanapata malipo kwa wakati wanapotekeleza miradi ya maendeleo ya umma.
Chama hicho kimesema kuwa uwepo wa sheria hiyo utasaidia kuweka utaratibu wa wazi wa malipo na kupunguza changamoto ya ucheleweshaji wa fedha, hali ambayo kwa sasa inaathiri uwezo wa kifedha wa makandarasi wengi wa ndani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 06, 2026 Mwenyekiti wa TUCASA, Qs Samuel Marwa amesema sheria hiyo inayojulikana kimataifa kama Security of Payment Act inaweza kusaidia kuweka mfumo wa kisheria unaolazimisha malipo ya kazi za ujenzi kufanyika ndani ya muda maalum pamoja na kuweka utaratibu wa haraka wa kutatua migogoro ya malipo.
Ameeleza kuwa ucheleweshaji wa malipo ya kazi zilizokamilika na kuthibitishwa umekuwa changamoto kubwa inayokwamisha ukuaji wa makandarasi wa ndani na kupunguza uwezo wao wa kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.
Marwa amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo, wakandarasi wengi hulazimika kukopa fedha katika taasisi za kifedha kwa riba kubwa ili kuendelea na utekelezaji wa miradi waliyopewa na taasisi za umma.
Kwa mujibu wa Marwa, hali hiyo huongeza gharama za miradi na wakati mwingine husababisha baadhi ya kampuni kushindwa kuendelea na shughuli zao au hata kufilisika kutokana na mzigo wa madeni unaotokana na kuchelewa kwa malipo.
Aidha, TUCASA imeeleza kuwa uzoefu wa kimataifa unaonyesha kuwa uwepo wa sheria kama hiyo husaidia kuimarisha mtiririko wa fedha katika sekta ya ujenzi na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi.
Amebainisha kuwa sheria kama hiyo tayari inatumika katika nchi mbalimbali zikiwemo Australia, Uingereza, Singapore na Malaysia ambapo imechangia kuimarisha sekta ya ujenzi na kulinda maslahi ya wakandarasi.
Chama hicho pia kimeipongeza Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa kuimarisha ushiriki wa makandarasi wa ndani katika miradi mikubwa ya maendeleo ya miundombinu nchini.
Pia kimetambua kauli ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba aliyoitoa Februari 15, 2026 mkoani Tanga alipokuwa akizungumza na wadau wa mradi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP), ambapo alisisitiza umuhimu wa kulinda fursa za makandarasi wa ndani.
Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alionya dhidi ya baadhi ya makampuni ya kigeni yanayotumia majina ya Watanzania kusajili kampuni ili kupata zabuni za Serikali kinyume na taratibu.
Hata hivyo, TUCASA imesisitiza kuwa kuanzishwa kwa sheria ya malipo pamoja na maboresho ya mifumo ya manunuzi ya umma kutasaidia kujenga sekta imara ya ujenzi, kuongeza ushindani wa haki na kuhakikisha makandarasi wa ndani wanashiriki kikamilifu katika maendeleo ya miundombinu na uchumi wa taifa.