MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Vanillah amepata shavu katika Kampuni ya kimataifa ya Apple Music ambapo ameingia katika mpango wao wa kushirikishwa na wasanii wengi wa kimataifa.
Kupitia Up Next Artist Development Program in East Africa, Vanillah ambaye mbali ya kuimba ni mwandishi wa mashairi atapata shavu la kushirikiana na wasanii kibao wa kimataifa.
“Najisikia furaha kuwa sehemu ya Apple Music’s Up Next, kwa sababu siyo kila mmoja anaweza kupata bahati kama hii.
“Ni kitu kizuri sana na inaonyesha ukuaji na ukomavu wa kazi yetu kuweza kufika kila kona ya dunia,” Vanillah anasema.
Anaongeza: “Kwa mashabiki zangu; naomba watarajie muziki mpya mzuri wenye ladha ya kipekee. Jitayarishe, kwa sababu utapokea maudhui ambayo utafurahia kweli.”
Vanillah alipata kutambuliwa kwa mara ya kwanza kama mtunzi wa nyimbo, alipoweka mkono wake katika wimbo wa Alikiba “Utu.”

Baada ya kushinda shindano la Super Nyota mwaka 2019, Vanillah alijiunga na Kings Music Records, na hivyo kuashiria mwanzo wa kazi bora zilizomuweka kwenye ramani ya muziki wa Bongo Fleva.
Vanillah anakwenda kung’ara zaidi kimataifa katika mpango wa Up Next Artist kwa kuingia kwenye orodha ya wasanii wengi duniani ndani ya playlist moja.
Baadhi ya mastaa watakaoshiriki kwenye mpango huo ni pamoja na 6lack, Daniel Caesar, H.E.R., Greta Van Fleet, Khalid, Amy Shark, Billie Eilish, Sabrina Claudio, Sigrid, Mr Eazi, Stefflon Don na Bad Bunny.
Wengine ni Juice WLRD, Bazzi, Jax Jones, NCT 127, Summer Walker, Tierra Whack, Dean Lewis, Pink Sweat$, Koffee, Megan Thee Stallion, Burna Boy, Clairo, Lunay naJessie Reyez.
Wasanii wengine ni Orville Peck, Victoria Monét, Ingrid Andress, Conan Gray, Don Toliver, Rema, BENEE, Holly Humberstone, Natanael Cano, Givēon, beabadoobee, Arlo Parks, Tate McRae, Foushee na Tems.
@@@