Global Publishers
March 6, 2026
0 Comments
Donald Trump amefanyiwa maombi maalum na wachungaji kadhaa katika ofisi ya Oval Office, wakimuombea hekima, uimara na uwezo wa kuliongoza taifa la Marekani.
Tukio hilo lilifanyika jana ambapo wachungaji hao walikusanyika ndani ya ofisi hiyo na kumzunguka rais huyo huku wakimuombea kwa pamoja. Baadhi yao walimwekea mikono wakati wengine wakinyanyua mikono yao kama ishara ya baraka na maombi.
Katika maombi hayo, mmoja wa wachungaji alisikika akisema:
“Bwana mpe uimara anaouhitaji ili aweze kuliongoza taifa letu kubwa.”
Maombi hayo yalilenga kumuombea Rais Trump apate hekima, nguvu na uongozi thabiti katika kuongoza nchi hiyo wakati wa changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa hilo.
Tukio hilo limeibua mjadala katika mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watu wakiliona kama ishara ya imani na wengine wakijadili nafasi ya dini katika uongozi wa kisiasa nchini Marekani.