WAZIRI ULEGA: BARABARA YA TAMKO MAPINGA KUKAMILIKA

Na Khadija Kalili,Kibaha
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi ambaye pia ni Mhe.Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amesema kuwa barabara ya TAMCO Mapinga itakamilika katika msimu ujao wa fedha na kuwataka wananchi waendelee kuwa wastahmilivu na adha wanayoipitia sasa.

Waziri Ulega amesema hayo katika kikao cha siku moja cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Pwani(RRB/CR/01/2025/2026) kilichofanyika tarehe 4 Machi 2026 kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Barabara hiyo inayotoka TAMCO Kibaha hadi Mapinga ambayo pia inaunganisha Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kuwa ni muhimu sana iweze kukamilika katika kukuza uchumi na kurahisisha kazi za kila siku kwa jamii nzima.
Aidha amezitaja barabara zingine ambazo ziko katika mpango mkakati wa ujenzi kuwa ni Bagamoyo kwenda Mlandizi,Makofia hadi Mzenga na barabara ya Kibaha hadi Kiluvya pamoja na barabara zingine muhimu huku lengo likiwa kuunganisha Mkoa .
Waziri Ulega amesema kuwa atahakikisha barabara hizo anaziwekea fedha na zipate wakandarasi ili zianze kujengwa huku akisema atatoa kipaumbele kwa miradi mikubwa ya kimkakati yenye sura ya Kitaifa ukiwemo ujenzi wa barabara ya Kibaha ambayo kwa hatua ya awali itajengwa Kilomita 3.6 ambapo kukamilika kwake kutatoa sura nzuri na muonekano uliobora kwa Manispaa ya Kibaha ambayo ndiyo lango kwa Mikoa yote na nchi jirani.
Wakati huohuo Mbunge wa viti Maalum Kibaha Vijijini Mhe.Hawa Mchafu amesema kuwa barabara ya Kongowe – Soga inayoelekea katika Kituo cha Reli ya Mwendokasi( SGR) imekuwa ni kero na changamoto kubwa kwa wananchi wanaotumia barabara hiyo ya vumbi na kero umbali mrefu pia huwa mwiba zaidi hasa katika kipindi cha mvua.
“Tunaomba hii barabara ili iweze kukamillika ichukuliwe na TANROADS nasema hivi kwa sababu TARURA wamekua wakisuasua na kushindwa kwenda na kasi ya maendeleo ambayo wananchi wanatarajia.