Mtanzania ateuliwa katibu mkuu mpya wa EAC

Arusha. Mtanzania Balozi Stephen Mbundi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akichukua Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva.

Balozi Mbundi ametangazwa leo Jumamosi, Machi 7, 2026 katika Mkutano wa kawaida wa 25 wa wakuu wa nchi za EAC unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Aidha, Rais wa Uganda Yoweri Museveni amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akichukua mikoba kwa Rais wa Kenya William Ruto aliyemali muda wake.

Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili masuala ya ushirikiano wa kikanda, maendeleo ya kiuchumi na mustakabali wa jumuiya hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi