Arusha. Rais wa Uganda Yoweri Museveni amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kipindi cha kuanzia Machi 2026 hadi 2028, akichukua mikoba kwa Rais wa Kenya William Ruto aliyemali muda wake.
Museveni amechaguliwa leo Jumamosi, Machi 7, 2026 katika Mkutano wa kawaida wa 25 wa wakuu wa nchi wa EAC unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili masuala ya ushirikiano wa kikanda, maendeleo ya kiuchumi na mustakabali wa jumuiya hiyo.
Nchi nane wanachama wa EAC ambazo sasa ziko chini ya uenyekiti wa Museveni ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan kusini, DRC na Somalia.
Endelea kufuatilia Mwananchi