……..
Balozi wa mazingira wa kujitolea Moses Mwakibolwa amewahamasisha wananchi kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti ili kulinda ikolojia na kupunguza athari za uharibifu wa mazingira nchini.
Mwakibolwa amesema wananchi wanapaswa kujenga utamaduni wa kupanda miti kila kunapotokea unyevunyevu ardhini ili kuongeza kasi ya upandaji miti na kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Amesema miti ya kupanda inapatikana katika vitalu vya Tanzania Forest Services Agency (TFS) na kinachohitajika ni wananchi kutenga muda kupanda miti katika maeneo wanayoishi.
Akizungumzia uzinduzi wa Darasa la Mazingira, amesema mpango huo utazinduliwa tarehe 04 Aprili 2026 katika eneo la Boko CCM, Kata ya Bunju, Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake Aisha Mwakibolwa ameitaka Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) kushirikiana na serikali za mitaa na wananchi kabla ya kukata miti katika maeneo ya makazi, na badala yake kushiriki katika kampeni za upandaji miti ili kulinda mazingira.
