WANAWAKE SF GROUP WATUMIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE KUTOA MISAADA KIBAHA

VICTOR MASANGU,KIBAHA

Wafanyakazi wanawake wa kampuni ya SF group ya Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha maadhimisho ya siku ya mwananke duniani wameamua kutoa msaada wa vitu mbali mbali katika shule ya Sekondari Koka pamoja na kufanya matendo ya huruma katika vituo viwili vya kulelea watoto yatima vilivyopo Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Katika kuona umuhimu wa siku hiyo wanawake hao wa kampuni ya SF group katika kukuza sekta ya elimu wameweza kutembelewa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Koka sekondari iliyopo katika kata ya Sofu na kutoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo kompyuta tatu, madaftari, pamoja na taulo za kike ambazo zitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wanafunzi wa kike.

Akizungumza katika sherhe za maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika Jimbo la Kibaha mjini Mkurugenzi wa Rasirimali watu na utawala wa kampuni ya SF Group Marygoreth Faustine ambaye aliongoza na kundi la wanawake kutoka makampuni mbali mbali yaliyopo ndani ya Sf Group amesema kwamba dhamira yao kubwa ni kurudisha fadhila kwa jamii ikiwa sambamba na kusaidia kuinua sekta ya elimu na afya.

“Sisi kama wanawake wa SF Group tumeamua kuitumia siku hii ya kipekee ya maadhimisho ya mwananke duniania kwenda kutembelea baadhi ya maeneo yaliyopo katika Jimbo la Kibha mjini na kwamba tumetoa msaada wa vitu mbali mbali katika shule ya Koka sekondari ikiwemo Kompyuta tatu, taulo za kike, pamoja na madaftari na mahitaji mengine ya msingi ambayo yataweza kuwasaidia wanafunzi katika kuongeza kiwango cha ufaulu,” amesema Mariagoreth.

Pia Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba katika ziara hiyo wameweza kupata fursa ya kutembelea Zahanati ya Mwendapole na kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali katika wodi ya wakinamama na kuwakabidhi msaada wa vifaaa mbali mbali ambayo vitawasaidia wakinamama wajawazito pamoja na wale ambao tayari wameshajifungua.

“Tumeungana kwa pamoja na wanawake wote wa kampuni ya SF Group katika kusherekea maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani kwa kimsingi tumeweza kupata fursa ya kutembelea katika maeneo manne ambapo pia tumefanya matendo ya huruma katika vituo vya watoto yatima,” amebainisha Mkurugenzi Mariagoleth.

Pamoja na hayo walikwenda kutembelea kituo cha watoto yatima cha Fadhila kilichopo kata ya misugusugu pamoja na kituo kingine cha Shalom kilichopo kata ya Msangani na kufanya matendo ya huruma na kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali ikiwemo sabuni, sukari, unga, mafuta, sabuni za kufulia na kuogea, dawa za meno pamoja na vitu vingine vya msingi ambavyo vitaweza kuwasaidia wattoto hao.

Katika hatua Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba lengo kubwa la kwenda kutoa msaada katika maeneo mbali mbali ya Jimbo la Kibaha mjini ni kwa ajili kuonyesha ushirikiano wa pamoja kati yao na jamii amabayo inawazunguka ikiwa pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuleta chachu ya maendeleo na kuisaidia jamii katika mambo mbali mbali ikiwemo afya, elimu, pamoja na huduma za kijamii.

Naye mwalimu mkuu wa shule ya Koka Sekondari Magreth William aliwashukuru kwa dhati wanawake hao wa kampuni ya SF Group kwa msaada huo ambao wameutoa pamoja na kumshukuru kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kutoa sapoti kubwa katika kuboresha sekta ya elimu katika maeneo mbali mbali ikiwemo shule hiyo ya Koka sekondari.

Nao baadhi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika vituo vya Fadhila na Shalom wametoa shukrani zao za dhati kwa wanawake wa kampuni hiyo ya SF Group kwa msaada huo kutoka kwa wanawake wa SF Group.

Wanawake wa kampuni ya SF Group wametumia kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kufanya matendo ya Huruma katika sehemu nne ikiwemo kituo cha watoto yatima cha Fadhila, Shalom, zahanati ya Mwendapole pamoja na kutoa msaada katika shule ya Koka sekondari.