WANAWAKE TTCL WAWASAIDIA WATOTO WAGONJWA WA MOYO JKCI

Baadhi ya Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakiwa na Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto – JKCI, Dk. Naizihijwa Majani (katikati) akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo hicho.
Baadhi ya Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakiwa na Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto – JKCI, Dk. Naizihijwa Majani (katikati mwenye miwani) akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo hicho.


Sehemu ya Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakikabidhi msaada kwa watoto wenye Matatizo ya Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) – jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Baadhi ya Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakiwa na Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto – JKCI, Dk. Naizihijwa Majani (katikati) akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo hicho.

Kulia baadhi ya wauguzi wa  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) – jijini Dar es Salaam, wakiwapatia maelezo baadhi ya Wanawake wa TTCL waliofika kituoni hapo kutoa misaada ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.


Sehemu ya Msaada uliotolewa na Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakiwa katika moja ya wodi za watoto kabla ya kugawa kwa wagonjwa.
Baadhi ya Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakigawa misaada hiyo kwa wagonjwa wa magonjwa ya Moyo kwa Watoto – JKCI.
Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto – JKCI, Dk. Naizihijwa Majani (kushoto) akizungumza na Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo hicho kabla ya kupokea msaada uliowasilishwa kituoni hapo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TTCL, Bi. Mercy Amani pamoja na Ofisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance.



Baadhi ya Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakipata huduma bure za uchunguzi wa magonjwa ya moyo JKCI mara baada ya kutoa msaada katika kituo hicho.


Na Joachim Mushi, Dar

WANAWAKE wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo wametoa msaada kwa watoto wenye Matatizo ya Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) – jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TTCL, Bi. Mercy Amani alisema wanaungana na taasisi nyingine na makundi mbalimbali kuadhimisha siku ya wanawake kwa kutambua changamoto wanazopata watoto wenye matatizo ya moyo JKCI pamoja na wazazi wao hivyo wameguswa kuwasaidia vitu kadhaa hospitalini hapo.

Alisema miongoni mwa vitu walivyokabidhi ni pamoja na Pampas (diapers), maziwa ya watoto wachanga kwa ajili ya watoto wanaopatiwa matibabu ya moyo hospitalini hapo na taulo za kike kwa ajili ya wazazi na walezi wanaouguza watoto wao katika Taasisi hiyo ya Magonjwa ya Moyo.

“…Kwa niaba ya Wanawake wa TTCL, tumefika hapa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuonesha mshikamano wetu na watoto wenye matatizo ya moyo pamoja na wazazi na walezi wao. Tunatambua kuwa safari ya matibabu hasa ya moyo si rahisi na ndio maana leo tumekuja si tu na msaada wa vifaa, bali pia na ujumbe wa faraja na matumaini,” alisema Bi. Mercy Amani akizungumza kwenye hafla hiyo.

” Kipekee tunapenda kuwapongeza na kuwashukuru madaktariwauguzi na wataalamu wote wa afya wa Taasisi hii kwa kazi kubwa ya kujitoa na ya huruma mnayoifanya kila siku kuokoa maisha ya watoto hawa. Huduma zenu ni tumaini kwa familia nyingi na mchango mkubwa kwa taifa letu,” alisisiotiza kiongozi huyo wa Wanawake TTCL.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto – JKCI, Dk. Naizihijwa Majani akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo hicho. alisema awali watu wengi walikuwa wakiamini magonjwa ya moyo ni kwa watu wazima tu lakini kwa sasa jamii itambue kuwa watoto wanaugua magonjwa ya moyo na magonjwa haya kwa watoto yapo ya kuzaliwa nayo na yanayokuja baadaye. 

Anabainisha kuwa wengi wa watoto wanaopatiwa matibabu katika kituo hicho ni wale wanaougua magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, huku takwimu zikioneshwa kuwa kwa kila watoto 100 wanaozaliwa mtoto mmoja hadi wawili wanazaliwa na tatizo la ugonjwa wa moyo. 

Aidha aliwataka wazazikuwa na utaratibu wa kuwachunguza watoto wao kiafya ili kama watagundulika mapema na matatizo hayo waweze kupatiwa matibabu mapema kabla ya kuathirika zaidi na mashambulizi ya ugonjwa.