KCB Bank Tanzania Yaunga Mkono Mageuzi ya Biashara na Fedha za Kidijitali EAC

Tarehe 07 Machi 2026.

KCB Bank Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Ndg. Cosmas Kimario, yashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.

Ushiriki huu unaangazia mchango wa benki katika majadiliano kuhusu maendeleo ya fedha za kidijitali, ukuaji wa masoko ya mitaji pamoja na urahisishaji wa biashara ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Uzinduzi wa “EAC Customs Bond” ni hatua muhimu katika kuimarisha biashara ya mipakani na kurahisisha shughuli za wafanyabiashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

#EACSummit

#Kcbbanktanzania

#forpeopleforbetter