Global Publishers
March 9, 2026
0 Comments
Ni simulizi ya kusikitisha lakini yenye tumaini. Mtoto Nuru alizaliwa katika mazingira ya kutisha ambayo si rahisi kuamini kwa haraka.
Inadaiwa kuwa mama yake alikuwa akikimbizwa hospitalini kujifungua pale ajali mbaya ilipotokea baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongwa na lori. Katika ajali hiyo, mama yake alifariki papo hapo, huku mtoto Nuru akitoka tumboni akiwa salama.
Tukio hilo lilishtua wengi na kuacha maswali mengi kuhusu jinsi mtoto huyo alivyoweza kunusurika katika mazingira hayo magumu.
Baada ya kupita mwaka mmoja tangu tukio hilo, waandishi wa Global TV Online wamemtembelea mtoto Nuru ili kufahamu maendeleo yake na hali anayoishi kwa sasa.
Licha ya mwanzo mgumu wa maisha yake, mtoto huyo anaendelea kukua vizuri, jambo linalowapa matumaini na faraja wale wanaomlea pamoja na jamii inayomzunguka.