Mwandishi wa habari Mwandamizi na Mkurugenzi wa Full Shangwe Media, Bw. John Bukuku akiaga mwili wa Mama yake Mzazi Anyambilile M. Kilindu katika ibada iliyofanyika Leo Machi 8, 2026 Madale, Dar es Salaam.
Mchungaji wa Kanisa la Moravian
Onesmo Kasyama akiongoza ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Anyambilile M. Kilindu.

……..
Mwili wa marehemu Bi. Anyambilile M. Kilindu, mama wa mwandishi wa habari mwandamizi na Mkurugenzi wa Full Shangwe Media, Bw. John Bukuku, umeagwa leo Machi 8, 2026 katika ibada iliyofanyika Madale, Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda Mbeya kwa ajili ya maziko.
Ibada ya kuaga mwili huo imehudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali waliokusanyika nyumbani kwa Bw. Bukuku kwa ajili ya kuifariji familia na kushiriki kumuaga mpendwa wao.
Baadhi ya waliohudhuria wameeleza masikitiko yao kwa kumpoteza marehemu huyo, wakisema katika maisha yake alijulikana kuwa mtu wa Mungu mwenye imani thabiti na upendo kwa watu.
Marehemu Anyambilile M. Kilindu alizaliwa Machi 22, 1930 mkoani Mbeya, na amefariki dunia Machi 7, 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi. Amina.