Global Publishers
March 11, 2026
0 Comments
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepokea taarifa ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zake.
Taarifa hiyo iliwasilishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma Machi 10, 2026 Bungeni Jijini Dodoma.
Baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Husna Sekiboko alisema hatua inayofuata ni kufanya ziara ya kuona utekelezaji katika miradi hiyo.
