TANESCO KUFANYA MABORESHO YA MFUMO WA LUKU

 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kutakuwa na maboresho ya mfumo wa manunuzi ya umeme (LUKU) yatakayofanyika kesho Jumatano usiku kuamkia Alhamisi kuanzia saa 6:00 usiku hadi saa 8:00 usiku (masaa mawili).

Kutokana na maboresho hayo, huduma ya kununua umeme kupitia mfumo wa LUKU haitapatikana kwa muda huo.

Hivyo, TANESCO inawashauri wateja wake kununua umeme mapema kabla ya muda wa maboresho ili kuepuka usumbufu wowote unaoweza kujitokeza.