UNICEF inasema watoto milioni 16 nchini Sudan wanateseka vibaya kutokana na vita

Alisema wengi wao wa huduma na vitisho vya ukatili vya kila siku, njaa, magonjwa na unyanyasaji wa kingono.

“Mapigano yanafanyika mbele ya milango yao, karibu na nyumba zao, shule zao na hospitali, na katika miji mingi na vijiji vya Sudan,” Catherine Russell, mkurugenzi mtendaji wa UNICEF, aliuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Amesema Watoto walio na umri wa chini ya miaka yao hatarini zaidi, ambapo zaidi ya milioni 1.3 wanaishi katika maeneo matano yanayokabiliwa na njaa nchini humo, na wengine milioni 3 wako katika hatari ya magonjwa ambayo kipindupindu, malaria na homa ya dengu kutokana na kudorora kwa mfumo wa afya.

Takriban vijana milioni 16.5 hawako shuleni.