NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini katika kukiimarisha chama imeamua kufanya ziara maalumu yenye lengo la kuwashukuru na kuwapongeza wanawake kwa umoja wao na mshikamao waliouonyesha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kupelekea chama cha mapinduzi (CCM) kuweza kushinda kwa kishindo katika nafasi za Udiwani, Ubunge pamoja na Urais.
Akizungumza katika ziara hiyo ambayo imefanyika katika Kata mbili za Visiga pamoja na Misugusugu Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Kibaha Elina Mgonja amesema kwamba wameamua kufanya ziara hiyo ambayo itaweza kuwapa fursa ya kukutana na wanawake hao ambao ndio walikuwa mstari wa mbele katika kukipigania chama kiweze kushinda na kupata viongozi wa CCM katika nafasi mbali mbali.’
Katika ziara hiyo ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji ambapo pia wametumia fursa ya kutembelea zahanati ya Misusugu pamoja na kuendesha zoezi la upandaji wa miti.
Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba wameamua kufanya ziara hiyo kwa lengo la kuweza kutoa shukrani kwa wanawake ikiwa pamoja na kuhamasiha viongozi wa matawi mbali mbali kuwezaa kushikamana kwa pamoja ili kuimalisha uwahi wa jumuiya pamoja na chama kuanzia ngazi za chini.
“Tumeanza ziara yetu ya jumuiya ya wanawake Wilayaa ya Kibaha ambapo tumetembeleakata mbili za visiga pamoja na kata ya Misugusugu lakini kitu kikubwa ni kwa ajili ya kuwashukuru wanawake wote wa chama cha mapinduzi pamoja na jumuiya wa UWT kwa kuweza kuwachagua viongozi kwa kura nyingi za kishindo katika nafasi ya Udiwani, Ubunge, pamoja na nafasi ya Urais,”amebainisha Elina
Kadhalika Mwenyekiti huyo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita kwa kuweza kutekeleza ilani ya cchama kwa vitendo ikiwemo kutenga fedha nyingi ambazo zimekwenda kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya, eilimu, maji, nishati ya umeme pamoja na huduma za kijamii.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Cesilia Ndalu amesema kuwa ziara hiyo pia imelenga kuanzisha vikundi vya uchumi ambavyo vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kukubwa kupambana na wimbii la umasikini.
Diwani wa kata ya Misugusugu Ally Simba amewahimiza wanawake wa UWT kuhakikisha wanachangamkia fursa za mikopo mbali mbali ambayo inatolewa na Halmashauri kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi pamoja na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika nyanja tofauti.
.jpeg)
.jpeg)
