CM YAMG’OA KIGOGO UWANJA WA MKWAKWANI

Na Oscar Assenga,TANGA

KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga imeagiza kusimamishwa kazi Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani Akida Machai kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyobainika wakati wa ziara ya kamati hiyo kwa ajili ya kujionekana maendeleo yake.

Akizungumza kuhusu maamuzi hayo ,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman ambapo alisema kwamba ukiangalia mapato yanayopatikana na gharama ambazo zinatumika zikitolewa sawasawa na CCM hakuna chochote kinachopatikana lakini maji yanalipwa na CCM ,Umeme unalipwa na CCM.

Alisema wanafanya hivyo kuhakikisha wananchi waendelee kupata burudani ya michezo sasa wanapotoa fedha na kuona mambo bado hawaendi kama wanavyotarajia ni jambo ambalo limekuwa likiwaumiza.

“Mimi Binafsi nilitoa milioni 50 inawezekana fedha hamtafiti nyie ndio maana hamuoni uchungu wake mimi natayetafutaa fedha kwa wadau anawawaomba anajua uchungu wake lakini wao kwa sababu hawajui uchungu wake na walimuweka yeye kama meneja wakiamini angeweza kutusaidia kuhakikisha uwanja huo muda wote unaweza kuwa bora unatumika”Alisema

“Lakini ukija wakati wote uwanja umekuwa kama Mbuga za Wanyama haiwezekani sio sawa mpaka leo viti vimeletwa havijafungwa na mmeviacha mpaka vimeota majani”Alisema

Aidha alisema kwamba wao wamekaa kama viongozi waliochaguliwa ili uwanja uweze kufikia vigezo lakini mpaka kufikia wakati uwanja kufungiwa na TFF hivyo hawawezi kukubali.

“Nilisema kwa hali ilivyo muda wowote TFF wangeweza kuja kutufungia uwanja hivyo nitoe maelekezo kwa Kamati ya Siasa mkoa kaeni Mtafute Meneja mwengine ili changamoto hizo ziweze kuondoka”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba kwa mpangaji Yule mwenye baa pale nje ambayo haijakidhi vigezo na Shirikisho la Soka nchini (TFF) walishasema ile baa inazuia washabiki kuingia uwanjani wakati wa mpira na inatakiwa kuondoka lakini mpaka leo haijaondoka.

“Maanake huyo mtu ana mapembe kiasi gani yeye ni mpangaji kwenye eneo letu lakini anakigomea CCM hivyo nahitaji hii baa leo iondoke ili maelekezo na maagizo ya TFF tuweze kuyatimiza na apatikane Meneja mwengine haraka ili aweze kushirikina na vongozi wa CCM kufungwa viti hivyo na nanatoa mwezi mmoja”Alisema

Awali akizungumza aliyekuwa Meneja wa uwanja wa CCM Mkoa wa Tanga Akida Machai alisema changamoto ya uhaba wa nguvu kazi ndio imepelekea kukwamisha viti hivyo kufungwa .

Alisema kwamba walikuwa wakihitaji kuongezewa nguvu kazi yeye anashukru CCM kwa nafasi waliompatia na wanamtakia kilala heri Meneja Mpya huku akieleza wakati viti vilipokuja walipeleka Bajeti ya kufunga viti CCM na vitu vinavyohusika na hawezi kutoa fedha zake kufungwa viti.