Na Mwandishi wetu- Dodoma
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imefanikiwa kuwajengea uwezo vijana 8,086 katika uendeshaji wa shughuli zinazohusisha kemikali, na kuwasaidia kulinda afya zao na mazingira, Mafunzo hayo yamewezesha vijana kupata fursa za biashara katika usafirishaji wa kemikali na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji wa bidhaa za kemikali.
Dkt Fidelice Mafumiko Mkemia Mkuu wa Serikali ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma katika Mkutano na Waandishi wa Habari kutangaza Miradi ya Maendeleo na fursa za vijana kwa mwaka 2025/2026
Mafumiko amesema Mamlaka imeendelea kuboresha miundombinu wezeshi, ikiwemo ujenzi wa majengo ya ofisi na maabara katika Ofisi ya Kanda ya Mashariki, jijini Dar es Salaam, wenye thamani ya Shilingi Bilioni 16.74, Ujenzi huo utaimarisha mazingira ya kufanyia kazi na utoaji huduma kwa wananchi.
Pia amesema Mamlaka hiyo imekamilisha ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika mipaka ya Rusumo, Kabanga, Mutukula, Holili, na Namanga, wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.13, Juhudi hizo zinakusudia kuboresha mazingira ya kazi na makazi kwa wafanyakazi.
“Miradi hii imewasaidia vijana 260 kupata ajira, ikiwemo wataalam 27 na vibarua 233. Mamlaka inaendelea kuunga mkono sera za Serikali zinazohusiana na matumizi ya rasilimali za ndani (Local Content)”
Aidha Mafumiko amesema Mamlaka imeajili vijana 58 katika kazi za usafi wa mazingira na 38 katika ulinzi wa mali na majengo ya Mamlaka, hiyo inaonyesha jitihada za kuunda mazingira bora ya ajira kwa vijana.
Hata hivyo Katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA, Mamlaka imeendelea kuboresha mifumo mbalimbali ya TEHAMA, na kukuza fursa kwa vijana katika sekta ya teknolojia.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)