Wema Sepetu Amzawadia Whozu Ujumbe Mtamu wa Mapenzi

Global Publishers
March 11, 2026
0 Comments

Mrembo na msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu, amemuonyesha wazi mapenzi yake kwa mpenzi wake, Whozu, kupitia ujumbe wa kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Wema alimtakia Whozu heri ya kuzaliwa huku akiambatanisha na maneno ya mahaba yaliyoonyesha namna anavyomthamini katika maisha yake.

Katika ujumbe huo, Wema aliandika:

“Happy Happy Happy Birthday shunu wa mama ❤️❤️❤️… Mi nakupenda bwana… Itoshe kusema… Kwani si uliumbwa kwa ajili yangu…???”

Ujumbe huo umevutia mashabiki wengi wa wawili hao, ambao wameendelea kuonyesha upendo wao hadharani licha ya changamoto zinazoweza kujitokeza katika mahusiano.

Sasa mashabiki wanasubiri kuona kama Whozu atajibu vipi ujumbe huo wa mahaba kutoka kwa Wema Sepetu.