Global Publishers
March 12, 2026
0 Comments
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Machi 11, 2026 amefunga mkutano wa uhakiki wa rasimu ya Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI-II) kwa ngazi ya Wakuu wa Mikoa.
Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI-II) ni maalumu na umeanzishwa na Serikali ili kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuvutia wawekezaji nchini.

Mpango huu ni nyenzo muhimu ya kuhakikisha kuwa kila sekta, kwa nafasi yake, inatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji. Mpango huu unalenga kuendeleza mafanikio yaliyopatikana, kuondoa vikwazo vilivyosalia na kupunguza gharama za kufanya biashara.
Vilevile, unalenga kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali na kuweka malengo yanayopimika katika kupunguza muda wa utoaji wa huduma.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma.

