Global Publishers
March 13, 2026
0 Comments
Ripoti mpya imeeleza kuwa Kiongozi mpya wa Iran, Mojtaba Khamenei, anadaiwa kuwa katika hali ya koma hospitalini na hajui kinachoendelea kuhusu vita vya Mashariki ya Kati wala kwamba ameteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo.
Mojtaba mwenye umri wa miaka 56 alichukua nafasi ya baba yake, Ali Khamenei, baada ya kuuawa katika shambulizi lililoripotiwa kutokea Februari 28.
Kwa mujibu wa chanzo kilichonukuliwa katika ripoti hiyo, Mojtaba anapatiwa matibabu katika Sina University Hospital jijini Tehran, huku akidaiwa kuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na sehemu kubwa ya hospitali hiyo kufungwa kwa ulinzi mkali.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa kutokana na hali yake, Mojtaba hajui kuhusu vita vinavyoendelea, kifo cha baadhi ya wanafamilia wake, wala uteuzi wake kama Kiongozi Mkuu wa Iran.
Ripoti nyingine pia ilidai kuwa majeraha yake ni makubwa na huenda alipata majeraha hayo wakati wa mashambulizi ya anga, ingawa haijathibitishwa wazi kama ni shambulizi lile lile lililosababisha kifo cha baba yake.