Global Publishers
March 13, 2026
0 Comments
Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa ndege yake ya kijeshi imeanguka nchini Iraq. Kwa mujibu wa taarifa ya U.S. Central Command, ndege ya kujaza mafuta angani aina ya Boeing KC-135 Stratotanker ilianguka baada ya kutokea tukio lililohusisha ndege mbili angani.
Jeshi hilo limesema tukio hilo halihusiani na mashambulizi ya adui wala moto wa kirafiki, huku likiongeza kuwa operesheni za uokoaji zinaendelea katika eneo la magharibi mwa Iraq, linalotajwa kuwa anga salama (friendly airspace).
