Gharama za Vipimo vya DNA Zapanda, Serikali Yazungumzia Changamoto
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amesema kuwa gharama za kufanya vipimo vya vinasaba vya binadamu (Human DNA) zimeongezeka kutoka shilingi 100,000/= kwa sampuli moja hadi kufikia shilingi 212,000/= kutokana na gharama za mchakato wa vipimo hivyo. “Gharama kwa sampuli moja ni 212,000/=. Kwa kesi ya baba, mama na mtoto gharama inazidisha mara tatu….