Shigongo Aungana na Wananchi Buchosa Kumuaga Juma Maanda

Global Publishers
March 14, 2026
0 Comments

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, ametoa pole kwa familia ya marehemu Juma Maanda aliyefariki dunia, alipofika kuwafariji ndugu na jamaa pamoja na kuhudhuria maziko yaliyofanyika katika Kijiji cha Bupandwa Village, Kata ya Bupandwa Ward ndani ya Jimbo la Buchosa Constituency.

Akizungumza katika maziko hayo, Shigongo aliwaomba wananchi kuendelea kumtumaini Mungu katika kila wakati wa maisha yao, akisisitiza kuwa wanadamu wote ni waja wa Mungu na kwamba maisha yana mwisho.