KUTORUHUSU bao lolote dhidi ya TRA United katika mechi nne za Ligi Kuu Bara walizokutana, zinaipa Simba matumaini ya kuendeleza ubabe wao katika mechi hii yenye rekodi ya kupatikana mabao kuanzia mawili.
Timu hizo zinakutana leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha saa 10:00 jioni, huku zote zikiingia uwanjani zikiwa zimetoka kushinda mechi zao za mwisho.
TRA United iliichapa Namungo mabao 2-0, huku Simba nayo ikiifunga Singida Black Stars mabao 2-1.
Katika mechi ya leo, mtihani wa Kocha Ettiene Ndayiragije ni kuhakikisha kikosi chake cha TRA United kinatikisa nyavu za Simba Simba kwa mara ya kwanza sambamba na ushindi juu yake.
Rekodi zinaonyesha kwamba, Simba katika mechi nne dhidi ya TRA United tangu inaitwa Tabora United, imeshinda zote bila ya kuruhusu nyavu zake kutikiswa, huku ikifunga mabao 11.
Matokeo ya mechi hizo msimu wa 2023-2024 yalikuwa hivi; TRA 0-4 Simba na Simba 2-0 TRA, kisha 2024-2025 ilikuwa Simba 2-0 TRA na TRA 0-3 Simba.
Wakati Ndayiragije akiwa na mtihani huo, Kocha wa Simba, Steve Barker, anahitaji kuendeleza rekodi hiyo bora dhidi ya TRA United wakati huu ambao anapambana kukipeleka kikosi chake nafasi ya juu zaidi kutoka ya nne kilipo sasa.
Simba inayoshika nafasi ya nne na pointi 27 katika mechi 12, imeachwa nane na kinara Yanga yenye 35, huku TRA United ni ya tisa na pointi 19 iliyocheza mechi 14.
TRA ina wachezaji ambao wamepita Simba akiwamo kiungo Nassor Kapama na mabeki Valentin Nouma na Chamou Karaboue, hivyo ni wazi wanaweza kuonyesha ushindani mkubwa kudhihirisha ubora wao.
Kwa mujibu wa Ndayiragije, hakuna mchezaji watakayemkosa katika mechi hii, hivyo Chamou ambaye anacheza hapo kwa mkopo, anaweza kukabiliana na Simba.
Ndayiragije, amesema: “Hatuna majeruhi, hivyo hakuna mchezaji ambaye tutamkosa kesho. Simba ni timu ambayo ipo kwenye ligi, tulijua mchezo huo utakuwepo kwa hiyo tumejiandaa vizuri na vijana wangu wapo tayari.”
Kocha Barker amesema: “Kikosi chetu kinazidi kuimarika na tunahitaji kupata ushindi kwenye mechi zetu. Kuhusu mchezo dhidi ya TRA United tupo tayari na hatuna majeruhi
