Trump Aitaka Uingereza Kutuma Meli za Kivita Kulinda Mlango wa Bahari wa Hormuz

Global Publishers
March 15, 2026
0 Comments

Rais wa Marekani, Donald Trump ameitaka Uingereza na mataifa mengine kutuma meli za kivita katika mlango bahari wa Strait of Hormuz ili kusaidia kulinda njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa bidhaa kutoka Mashariki ya Kati dhidi ya mashambulizi ya Iran.

Trump amesema anatarajia pia China, Ufaransa, Japan na Korea Kusini zitatuma meli zao katika mlango huo wa bahari, ambako meli kadhaa za mafuta zinaripotiwa kushambuliwa tangu Marekani na Israel zilipoanzisha vita dhidi ya Iran takribani wiki mbili zilizopita.

Ikijibu kauli za Trump, Uingereza imesema inajadili ‘chaguzi mbalimbali za kuhakikisha usalama wa usafirishaji wa baharini katika eneo hilo’ kwa kushirikiana na washirika wake.

Kwa upande wake, Tehran imesema itaendelea kuzuia njia hiyo ya bahari, ambayo ndiyo njia yenye shughuli nyingi zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta, ambapo takribani asilimia 20 ya mafuta yote ya dunia hupita hapo kwa kawaida.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.