******
Afisa habari wa chama cha makocha wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania TPBCA, Dauka Somba amefanya kikao na makamu mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania, TPBRC, Jacob Mbuya.
Somba na Mbuya wamefanya kikao hiko leo katika ofisi za TPBRC zilizopo Ilala jijini Dar es salaam lengo likiwa ni kuandaa mikakati ya kuboresha mchezo wa ngumi za kulipwa Tanzania kwa kushirikisha mamlaka hizo zote mbili yaani kamisheni na TPBCA.
Hii ni mara ya kwanza kwa Somba kukutana na uongozi wa TPBRC tangu atangazwe kuwa afisa habari wa TPBCA mwanzoni mwa juma hili.