MELI NNE ZA MIZIGO KUIPAISHA TANZANIA

……

Kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa meli nne kubwa za mizigo katika Bandari ya Karema ni fursa kwa wananchi wa mikoa inayopitiwa na Ziwa Tanganyika ya Rukwa, Katavi, Kigoma na kuongeza kipato cha kaya na Taifa.

Ujenzi wa meli hizo ulianza rasmi Aprili 2025 na ukitarajiwa kukamilika Julai 2026. Mpaka sasa mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 95 huku meli zote zikiwa majini kwa hatua mbalimbali za uhakiki wa mwisho kuanza kutoa huduma.

Oktoba 2023, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ilipokea maombi kutoka Kampuni ya Gold Voyage Logistics Limited, kampuni tanzu ya Zijin Mining Group Co. Ltd kutoka China ikiomba kukodishwa eneo katika Bandari ya Karema ili kujenga meli hizo.

Msimamizi Msaidizi wa Bandari ya Karema, Anthony Poyo amesema hayo wakati wa tukio la kuingizwa majini kwa mara ya kwanza meli ya nne zinazotarajiwa kutoa huduma nchi za DR Congo, Zambia, Burundi na Tanzania.

Amebainisha kuwa meli hizo zitakuwa kiichocheo cha usafirishaji wa madini kama ya lithium, shaba na dhahabu kutoka eneo la Manono nchini DRC yanayochimbwa na kampuni hiyo ambapo kupitia Manono, Bandari ya Kalemie hadi Bandari ya Kigoma, Dar es Salaam na Tanga zitatumika kabla ya kusafirisha Kwenda nje ya nchi.

Mei 12, 2025, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile alifanya ziara Karema kujionea ujenzi wa meli hizo zitainufaisha zaidi Tanzania kwani usafirishaji wa shehena ya mizigo kutoka Bandari ya Kigoma unategemea kutumia miundombinu ya reli zilizopo za MGR na SGR hadi Bandari ya Dar es Salaam na Tanga.

Meneja Rasilimali Watu kutoka Kampuni ya Ankola Shipyard Co. Ltd ambao ndiyo waliounda meli hizo, Mohammed Mohamed Chande amesema mradi huo ulianza April mwaka jana na ulitarajia kukamilika Julai mwaka huu.

Baadhi ya wananchi wamepongeza hatua hiyo ya kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo kwani shughuli zao za kilimo, uvuvi na mifugo huenda ikapata masoko ya ndani na nje kwani usafirisaji utakuwepo.

“Tunamwomba Rais aweke msukumo kwenye ujenzi wa barabara, kama ambavyo bandari imekamilika nayo ikamilike ili usafiri na usafirishaji iwe mzuri na sisi wananchi tunufaike zaidi,” amesema Sarafina Kambi mkazi wa Kirema.