Na Mwandishi Wetu
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohammed Said Mohammed (DIMWA), amewahimiza viongozi na wanachama wa Chama hicho kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini, sambamba na kushiriki kikamilifu katika kukijenga na kukiimarisha chama.
Ametoa mwito huo alipokuwa akizungumza katika hafla ya futari ya pamoja aliyoiandaa katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, iliyohudhuriwa na viongozi, wanachama pamoja na wageni waalikwa, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mshikamano na kuimarisha mahusiano ndani yaCCM Zanzibar.
Akizungumza wakati wa futari hiyo Dkt. Dimwa amesisitiza kuwa mshikamano na nidhamu ndani ya chama ni nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya kisiasa na maendeleo ya taifa.
Ameongeza katika kipindi hiki, ni wajibu wa kila mwanachama ni kuhakikisha anakuwa balozi mzuri wa amani, hasa kwa kuzingatia kuwa CCM imejijengea sifa ya kuongoza kwa misingi ya utulivu na mshikamano wa kitaifa.
Dk.Dimwa amewataka pia viongozi kuendelea kuwa karibu na wananchi, kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati ili kuimarisha imani ya wananchi kwa chama hicho.
.jpeg)





.jpeg)

