Dosari za kisheria zafuta hukumu miaka 30 jela, kesi kuandikwa upya


Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Simiyu, imebatilisha hukumu ya kifungo cha miaka 30 aliyokuwa amehukumiwa Majingwa Ndushi baada ya kubaini kasoro za kisheria katika namna hukumu ilivyotolewa na mahakama ya chini. Mahakama imefuta hukumu yote na kuamuru kesi irejeshwe Mahakama ya Wilaya ya Meatu kwa ajili ya kutoa hukumu upya kwa mujibu wa sheria.