MBUNGE BUKOBA MJINI ATOA MSAADA KWA MAKUNDI MAALUM,WANUFAIKA WA TASAF

Na Diana Byera,Bukoba

MBUNGE wa Jimbo la Bukoba Mjini, Johnston Mutasingwa ameendelea kugusa maisha ya wananchi kwa vitendo baada ya kutoa msaada kwa makundi maalum pamoja na wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)  katika Kata ya Kibeta katika kipindi iki cha Mfungo wa Kwalezima na Ramadhan

Msaada huo umekabidhiwa leo Machi 18,2026  kupitia Katibu wake Hamada Simba ambaye amesema  Mbunge kwa sasa yupo nje ya jimbo akiendelea na majukumu ya ubunge lakini  bado anawajali wananchi wake na kuhakikisha wanapata msaada wa  mahitaji katika kipindi hiki Cha Mfungo 

Amesema msaada huo unalenga kuwasaidia wananchi walio katika mazingira magumu, wakiwemo wazee, watu wenye ulemavu pamoja na kaya zenye kipato cha chini zinazofaidika na mpango wa TASAF.

Mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na chakula sukari Sabuni na Vyakula mbalimbali vya kusaidia katika  familia hizo katika Mfungo.

Kwa upande wao wananchi ambao wamenufaika na msaada huo wameonesha furaha na kutoa shukrani zao za dhati kwa Mbunge wao, wakieleza kwamba hatua hiyo imewapa faraja kubwa na kuwasaidia kukabiliana na changamoto za maisha ya kila siku.

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutujali,Msaada huu umekuja wakati sahihi na utatusaidia sana katika maisha yetu,” amesema mmoja wa wanufaika.

Wakati huo huo Diwani wa Kata kibeta  AnaStella Alphuns amesema kwa ujumla, tukio hilo limeendelea kuonesha mshikamano kati ya viongozi na wananchi pamoja na juhudi zinazoendelea za kuhakikisha ustawi wa jamii unaimarika, hasa kwa makundi yenye uhitaji zaidi.