Yas Yaendelea Kuwa Kinara Yashinda Tuzo, Mtandao Wenye Kasi Tanzania

Kampuni ya kimataifa ya uchambuzi wa mitandao, Ookla, imethibitisha tena ubora wa mtandao wa Yas baada ya majaribio mengi ya spidi kwa mujibu wa matokeo ya Speedtest kutoka Ookla.

Dar es Salaam, Tanzania – 18 Machi 2026 – Yas Tanzania, Kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali nchini ambayo pia ni sehemu ya Axian Telecom Group kwa mara nyingine tena imetambuliwa kama mtandao wenye kasi zaidi nchini, hii ikiwa ni mara ya tatu mfululizo kwa kampuni kutwaa tuzo hiyo kwa mujibu wa matokeo ya Speedtest Award kutoka Ookla.

Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa kongamano la teknolojia duniani, ‘Mobile World Congress’ (MWC) 2026, lililofanyika Barcelona, ikitambua ubora wa mtandao wa Yas kwenye kasi na huduma ya mawasiliano ya uhakika kote nchini.

Tuzo hii inatokana na mamilioni ya majaribio yaliyofanywa na watumiaji kupitia jukwaa la Speedtest, ambalo hupima utendaji halisi wa mitandao, ikiwemo kasi ya kupakua na kupakia, katika mitandao yote mikubwa ya simu nchini. Katika kipindi cha tathmini, Yas iliongoza kwa kupata Speed Score ya juu kuliko mitandao mingine yote ya hapa nchini.

Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Pierre Canton Bacara, Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Tanzania, alisema utambuzi huo unaakisi dhamira ya kampuni katika kujenga miundombinu ya kisasa ili kutoa uzoefu bora wa huduma za kidijitali kwa watanzania.

“Kushinda tuzo ya Ookla kwa miaka mitatu mfululizo ni jambo la kujivunia kwa Yas na kunathibitisha nafasi yetu kama kipimo cha ubora wa huduma za mitandao ya simu nchini. Katika miaka michache iliyopita, tumefanya uwekezaji mkubwa wa kuboresha na kupanua miundombinu ya mtandao, jambo lililotuwezesha kuwa na mtandao mpana zaidi wa 4G na mtandao wa 5G unaokua kwa kasi nchini. Hii inahakikisha watanzania wengi zaidi, popote pale walipo, wanapata huduma ya mtandao wenye kasi katika kuwezesha masuala mbalimbali kama elimu, biashara, burudani na huduma za kifedha kidijitali.”

Kupitia maboresho ya mtandao na upanuzi unaoendelea, Yas imeimarisha huduma za mawasiliano Tanzania Bara na Zanzibar kwa kujenga vituo vipya, kuboresha miundombinu iliyopo na kutumia teknolojia za kisasa kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya huduma za intaneti ya kasi.

Stephen Bye, Rais na Afisa Mtendaji wa Ookla, Kampuni tanzu ya Ziff Davis, alisema: “Mafanikio ya Yas kushinda tuzo za Speedtest kama mtanado wa simu wenye kasi zaidi, mwaka baada ya mwaka, ni uthibitisho wa uongozi wao katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania. Tuzo za Speedtest zinatambulika kwa uchambuzi makini na usio na upendeleo, na hivyo kufanya mafanikio haya kwa nusu ya pili ya mwaka 2025 kuwa ya kipekee. Tuzo hii inaonyesha dhamira ya Yas ya kutoa huduma bora ya mtandao kwa wateja wake.”

Uwekezaji endelevu wa kampuni katika miundombinu ya kisasa unaendelea kubadilisha namna ambayo watanzania wanawasiliana, kujifunza, kufanya kazi na kushiriki katika uchumi wa kidijitali. Kupitia huduma thabiti za 4G na upanuzi wa 5G katika maeneo ya kimkakati, Yas inawezesha utiririshaji wa maudhui kwa kasi, matumizi bora ya majukwaa ya kidijitali, kuboresha mazingira ya elimu mtandaoni na kuwapa wafanyabiashara na mtu binafsi huduma ya uhakika na yenye ufanisi.

Utambuzi huu mpya unaimarisha zaidi dhamira ya Yas Tanzania katika kuiwezesha jamii na kuharakisha mabadiliko ya kidijitali nchini kwa kutoa huduma za mawasiliano kwa kiwango cha kimataifa ili kukidhi mahitaji wateja wake ambayo yanabadilika kila siku.