Global Publishers
March 19, 2026
0 Comments
Kwenye upepo mwanana wa Coco Beach, kumezaliwa tabasamu mpya kwa kina mama wanaochangamsha jiji la Dar es Salaam kwa vyakula vyao vitamu. Meridianbet imewasili na zawadi za aproni ikiwa ni ishara ya heshima kwa juhudi za Mama Lishe wanaopambana kila siku kujitafutia kipato na kuhudumia mamia ya wateja ufukweni hapo.
Hili halikuwa tukio la mara moja kwa Meridianbet, bali ni muendelezo wa dhamira yake ya kusimama bega kwa bega na wajasiriamali wadogo. Katika eneo hilo lenye pilika nyingi za biashara, kampuni ilichagua kugusa moja kwa moja maisha ya wanawake ambao ni injini ya uchumi na sehemu muhimu ya jamii ya wateja wao.
Vilevile, Michezo mingi zaidi ya kubashiri inaendelea kupatikana ndani ya Meridianbet ikiwa na ODDS kubwa na machaguo mengi zaidi. Kushiriki ni vyepesi kupitia tovuti ya MERIDIANBET au kwa kupiga *149*10#.
Kutoka Meridianbet, Nancy Ingram alisisitiza wazi kuwa kusaidia wajasiriamali wadogo si chaguo, ni wajibu. Alieleza kuwa wengi wa Mama Lishe ni wateja waaminifu wa Meridianbet, hivyo kampuni imeona ni muhimu kurudisha kwao kwa vitendo, kuwawezesha, kuwathamini na kuwapa motisha ya kusonga mbele.
Furaha ilitawala kila kona. Mama Lishe walipokea aproni hizo kwa shukrani kubwa, wakieleza kuwa msaada huo utarahisisha kazi zao na kuongeza hadhi ya biashara zao mbele ya wateja. Kwao, hii ilikuwa zaidi ya zawadi, ni ishara kwamba juhudi zao zinaonekana na kuthaminiwa.
Meridianbet inaendelea kuonyesha kuwa ushindi hauishii kwenye mkeka pekee. Ni kuhusu kugusa maisha, kujenga jamii na kufungua milango ya mafanikio. Ukiwa na Meridianbet, unakuwa sehemu ya zaidi ya burudani, unakuwa sehemu ya mabadiliko halisi.