Bakari Mahundu
March 19, 2026
0 Comments
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mjini, ameshiriki katika sherehe za uzinduzi wa Jimbo jipya la Kanisa Katoliki la Bariadi pamoja na usimikaji wa Askofu wa kwanza wa jimbo hilo, Mhashamu Prosper Baltazar Lyimo, zilizofanyika leo Alhamisi, tarehe 19 Machi 2026.

Katika hafla hiyo, Mhe. Kundo alimshukuru Papa Leo XIV kwa kukubali kuanzishwa kwa Jimbo jipya la Katoliki la Bariadi na kuridhia kusimikwa kwa Askofu wa kwanza wa jimbo hilo, hatua inayolenga kusogeza huduma za kiroho karibu zaidi na wananchi wa Mkoa wa Simiyu.
Alisema kuanzishwa kwa jimbo hilo kutasaidia kuimarisha maadili ya jamii na kuleta mwanga wa imani, tumaini na upendo miongoni mwa wananchi.