Global Publishers
March 19, 2026
0 Comments
Simba imeshindwa kuibuka na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Katika mchezo huo, Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Anicet Oura dakika ya 32, kabla ya Pamba Jiji kusawazisha dakika ya 35 kupitia kwa Mwashinga.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha sare yao ya nne msimu huu, na sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 28 baada ya kucheza mechi 13. Wababe hao wa Msimbazi wako nyuma kwa alama 9 dhidi ya vinara Young Africans SC, ambao wana michezo miwili zaidi.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Mashujaa FC walitoka sare ya bila kufungana (0-0) dhidi ya Azam FC.
Matokeo Kamili:
Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC
Mashujaa FC 0-0 Azam FC