Global Publishers
March 20, 2026
0 Comments
Waislamu nchini Tanzania kesho Machi 21, 2026 wanatarajiwa kuadhimisha Sikukuu ya Eid El-Fitri kwa shangwe na ibada maalum, ikiwa ni hitimisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Nchini Tanzania, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika Baraza la Eid litakalofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa BAKWATA, Alhaj Nuhu Mruma, hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), kuanzia saa 9:00 alasiri, ambapo viongozi mbalimbali wa dini na serikali pamoja na waumini watashiriki.
Baraza hilo la Eid ni sehemu muhimu ya maadhimisho ya sikukuu hiyo, likiwa jukwaa la kuhimiza mshikamano, amani na maadili mema katika jamii.